
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. George Simbachawene.
Akiongea Bungeni Jana Waziri wa TAMISEMI,Mhe. George Simbachawene, amesema kuwa kumekua na tabia ya baadhi ya askari kuwanyanyasa wafanyabiashara hao kwa vigezo vya kutoza ushuru pamoja na kutokuwepo katika maeneo stahiki ya biashara.
Mhe. Simbachawene amesema wafanyabiashara hao ndio walipaji wa kubwa wa kodi ambazo zinaisaidia serikali katika kuleta maendeleo ingawa wengi wao hawapo katika mfumo rasmi wa kibiashara.
Waziri huyo wa Tamisemi amekiri kuwa Serikali imekosa mfumo sahihi wa utozaji ushuru kwa wafanyabishara hao ikiwa ni pamoja na kutotenga maeneo maalumu kwa ajili ya biashara zao hali inayowapelekea kunyanyasika na Askari Mgambo katika miji tofauti.
Waziri Simbachawene amezitaka Mamlaka zote za mijini zinazounda majeshi ya Mgambo chini ya sheria ya Polisi kuhakikisha kuwa katika opresheni wanayoifanya inakua na makubaliano maalumu katika Mamlaka husika.
Amesema kuna haja ya serikali ya kufanya mapitio shiria hizo ili kuondoa adha hiyo ambayo inawafanya wananchi hasa wafanaybishara hao wadogo kuichukia serikali kutokana utaratibu uliopo sasa.