
Meya wa Ubungo, Boniface Jacob.
Meya Jacob ameyabainisha hayo leo Mei 8, 2020, na kueleza kuwa maisha na kazi zake zimekuwa na mashaka kuanzia Julai 2019, mara tu baada ya kubaini upotevu huo wa pesa uliofanywa na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo na kuongeza kuwa yeye pamoja na Madiwani wenzake watakuwa tayari kuhojiwa na kutoa vielelezo vyote.
"Napenda kutoa wito kwa Rais Magufuli, ambaye mara zote yeye amejipambanua kwamba ni kiongozi jemedari na shujaa wa vita vya ufisadi, kuingilia kati suala hilo kwa kutumia vyombo vya uchunguzi kwa ajili ya ufuatiliaji wa kina, katika mjadala wetu wa kubaini wizi wa Bil 1.6, katika Baraza lile tulikuwa na vyombo vya usalama, hivyo wanaweza wakaanza kuvihoji vyombo vile kama wataona mimi naongea haya kwa maslahi yangu ya Udiwani na Umeya" amesema Meya Jacob.
Aidha Meya Jacob ameongeza kuwa jambo la kuondolewa katika nyadhifa zake zote si la kisiasa bali ni la maslahi binafsi ya genge la watu akiwemo Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo.