Jumatatu , 12th Oct , 2020

Kampuni ya kubashiri matokeo ya Meridian Bet na klabu ya Lions, zimesaidia kampeni ya upimaji,matibabu na ushauri nasaha ya magonjwa ya macho, sukari na shinikizo la damu, yaliyotolewa bure kwenye hospitali ya Polisi Kilwa road, Jijini Dar es Salaam.

Wawakilishi wa Kampuni ya Meridian Bet na Kampuni ya klabu ya Lions

Akizungumza wakati wa Zoezi hilo likiendelea Mganga mkuu wa hospitali hiyo na mkuu wa kikosi cha afya cha polisi nchini, Dk Hussein Yahya alisema muitikio wa Watanzania waliojitokeza kupatiwa huduma hiyo umekuwa mkubwa tofauti na ilivyotarajiwa.

Amesema zaidi ya watu 456 walijitokeza kupatiwa huduma hiyo wakiwamo watoto na wazee, huku Kamishna msaidizi wa jeshi la Polisi, Kihenya Kihenya akiwaomba wadhamini wao, kampuni ya Meridian Bet na klabu ya Lions, kampeni hiyo kuwa endelevu.

Kwa upande wake Meneja Uendeshaji wa Meridian Bet, Carlo Njato amesema wameamua kusaidia kampeni hiyo kama sehemu ya kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali katika sekta ya afya huku  Gavana wa klabu ya Lions Tanzania, Moiz Bakari alisema klabu yao imekuwa ikijitoa kwa jamii na hiyo ni sehemu ya majukumu wanayoyafanya.

Alisema hiyo ni mara nyingine tena kwa kampuni yao wakishirikiana na Lions Club kusaidia jamii yenye uhitaji.

Tulifanya hivi kwenye hospitali ya wazee Kinyerezi, pia wakati wa maadhimisho ya ugonjwa wa kansa duniani, tulitembelea na kuwafariji wagonjwa katika Taasisi ya Kansa ya Ocean Road Dar es Salaam.