
Kushoto ni picha ya uopoaji na kulia ni Mbunge wa Ukerewe Joseph Mkundi
Akiongea na www.eatv.tv ameweka wazi kuwa Kivuko hicho kilifanyiwa ukarabati miezi miwili iliyopita, hivyo kilikuwa sawa na kilikuwa mbioni kubadilishiwa ratiba ikiwemo kuongeza idadi ya safari ili kukidhi mahitaji ya wananchi wa eneo hilo.
''Kuhusu hoja yangu niliyoitoa bungeni, ilifanyiwa kazi ambapo tulikuwa tunahitaji injini mbili ambazo zilipatikana na zikafungwa labda tu suala ambalo lilikuwa bado tunalifanyia kazi ni kuona namna gani tunaweza kubadilisha idadi ya safari'', amesema.
Aidha Mbunge huyo amesema yeye mwenyewe ni miongoni wa watu waliopoteza ndugu katika ajali hiyo ambapo amedai takribani ndugu zake watatu wamefariki kwenye ajali hiyo.
Pia ametumia fursa hiyo kutoa ushauri kuwa katika eneo la kisiwa kama hicho kuna uhitaji wa jeshi la wanamaji ambalo linaweza kuchukua hatua za haraka pale inapotokea ajali.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, mhandisi Isack Kamwelwe, amesema wanategemea ifikapo saa 12:00 jioni watatoa taarifa rasmi kuhusu zoezi la uopoaji wa miili kwenye ajali ya hiyo ya kivuko cha Mv Nyerere kilichozama jana huko Ukerewe.
Zaidi msikilize hapo chini akieleza zaidi.