
Bi. Chatanda ameyasema hayo katika kikao cha 45 mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma katika kipindi cha maswali kutoka kwa wabunge na majibu kutoka serikalini akisisitiza kwamba kutulia kwa vyama vingine kutawezesha chama kilichopo madarakani kutekeleza ilani yake kwa ufasaha.
Swali lake hilo likaungana na la mwenyekiti wa kamati ya maadili na madaraka ya Bunge George Mkuchika ambaye ameiuliza serikali kwa nini isitoe elimu kwa viongozi wa vyama vya siasa ili watambue kwamba ilani inayotawala ni ya CCM.
Akijibu swali hilo Jenista Joakim Mhagama ni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu amesema kwamba sheria zilizopo katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na utawala bora ndizo zitakazotumika katika kuendesha shughuli mbalimbali.
Aidha Waziri Mhagama amesisitiza kwamba kama kuna haja ya kufanya hivyo wadau watumie mchakato wa katiba unaondelea katika kufanya jambo hilo ila kwa sasa katiba itaendelea kufuatwa kama kawaida.