Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Zanzibar Mh. Said Ally Mbarouk.
Hayo yamezungumzwa na aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Mh. Said Ally Mbarouk na kuongeza kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa visiwani humo haina uhalali wa kikatiba kuendelea kuwepo kwani ilishamaliza muda wake.
Mh. Mbarouk amesema hawakubaliani na uamuzi was Dkt. Shein kuendelea kusalia madarakani na serikali yake yote wakiwemo wao na ndio maana wameamua kujiondoa lengo likiwa ni kuilinda Katiba ya Zanzibar.
Katika hatua nyingine baraza kuu la uongozi la chama hicho limetoa maazimio saba likiwemo kuitaka ZEC itengue uamuzi wa Jecha na kurudi kazini kukamilisha kazi ya kuhakiki matokeo ya uchaguzi wa majimbo 23 yaliyobaki.
Aidha baraza hilo limesema baada ya ZEC kutangaza mshindi wa uchaguzi wa urais wa Zanzibar Maalim Seif akutane na vingozi wa CUF na CCM waliopata wawakilishi kujadili uundwaji mpya wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.