Jumatatu , 7th Nov , 2016

Idadi ya mauzo katika Soko la Hisa la Dar es Salaam imeongezeka kwa asilimia 56 kutoka shilingi bilioni 5.3 had shilingi bilioni 8.3 kwa mujibu wa taarifa ya mwenendo wa biashara katika soko hilo kwa kipindi cha wiki moja iliyopita.

Patrick Mususa

 

Meneja Miradi na Uendelezaji Biashara wa soko hilo Patrick Mususa amesema katika kipindi hicho, idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imeongezeka mara mbili kutoka hisa 869,453 hadi hisa milioni moja na laki nane.

Mususa ameongeza kuwa ukubwa wa mtaji wa soko umepanda kwa asilimia 0.4 huku ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani pia ukiwa umepanda kwa asilimia 0.3 na kufikia shilingi trilioni 8.21 kutoka shilingi trilioni 8.19.