Jumatatu , 26th Sep , 2022

Mtu mwenye silaha ameishambulia shule moja iliyopo katikati mwa Urusi na kuua watu 13 na kujeruhi wengine 21 . 

Waliopoteza maisha ni  pamoja na wanafunzi saba ambao ni watoto wa shule hiyo yenye wanafunzi  takribani   1,000 katika jiji la Izhevsk.

Baadae mtu huypo aliamua kujiua mwenyewe kwenye eneo la tukio. Taarifa zinasema kwamba alikua ni mwanafunzi wa zamani wa shule hiyo . Kulikua na hali ya taharuki wakati tukio hilo linajiri. 

Baadhi ya picha zimeonyesha uwepo wa damu kwenye madarasa ikiwemo mabaki ya risasi kwenye madirisha. Mbali na watoto sita waliopoteza maisha, wamo watu wazima sita wakiwemo walinzi wawili wa shule . 

Mshukiwa wa tukio hilo ametambulika na uchunguzi umeanza kujua ni wapi alikua anaishi.  Kumetangazwa maombolezo ya mpaka tarehe 29  mwezi huu huku Rais wa nchi hiyo  Vladimir Putin akisema kwamba anasikitishwa na tukio hilo.