Jumatatu , 22nd Jan , 2024

Matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ikiwemo lugha mbaya dhidi ya viongozi zinazotolewa na vijana katika mitandao wakiwemo wahitimu wa taasisi za elimu ya juu na vyuo vikuu ni moja ya sababu inayotajwa kuwakosesha vijana kupata fursa ya kuaminiwa na kuteuliwa kushika nafasi za uongozi.

Akizungumza na wasomi hao katika tawi la chama cha Mapinduzi Taasisi ya Uhasibu Tanzania TIA Kampasi ya Mbeya Diwani wa kata ya Iyela  Jijini Mbeya Mussa Ismail  amesema tabia ya vijana kutumia mitandao ya kijamii tukana viongozi inawakosessha fursa za kuteuliwa kuwa viongozi huku Katibu wa siasa na ueneze mkoa wa Mbeya Christopher Luhagila amewataka wasomi hao kujitokeza  kuwania nafasi za uongozi katika chaguzi zijazo.

"Hatufanikiwa wakati mwingine matumizi mabaya ya mitandao wakati mwingile kauli mbaya kwa viongozi wetu ndizo zinazo tukwamisha kupata fursa ya kuteuliwa kuwa viongozi  kufanya hivyo kuna kukosesha sifa za kuaminiwa  kuwa kiongozi" Mussa Ismail, Diwani Kata ya Iyela

"Vijana wasomi mkagombee nafasi na huko ndiko waliko watu na mimi niwaahidi tutawapa ushrikiana tuanataka viajana tuwepe dhamani ili na wao waweze kushiriki na sisi kuijenga nchi yetu" Chritopoher Luhagila, Katibu Itikadi na Uenezi CCM Mkoa wa Mbeya

Awali wakisoma taarifa ya  Tawi la Chama cha Mapinduzi  Taasisi ya Uhasibu Tanzania TIA Kampasi ya Mbeya  Mjumbe wa UVCCM Said Athuman Kapuya amesema tawi lao wamebuni mradi wa kudurusu karatasi lakini wanakabiliwa na changamoto ya mtaji hivyo wanamuomba  Mwenyekiti  Chama Mkoa wa Mbeya Patrice Mwalunenge  awasaidia ambapo  amekubali kutoa zaidi ya shilingi milioni nane ili mradu huo uanze kufanya kazi.

"Makadilio ya mradi huo wa stesheni ni juma ya zaidi ya shilingi milioni kumi na moja na hadi sasa tumefanikiwa kukusanya mataji wa shilingi milioni mbili na laki tano kwa ajili ya kununua samani kama vile viandiko na viandikio pia pesa kwa ajili ya kulipia pango la chumba cha biashara Said Athuman Kapuya"  Mjumbe wa Uvccm TIA Mbeya

"Andiko lenu mmeliandika kisomi hivyo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi amenituma niwambie kwamba amekubali kumalizia kiasi kilicho baki ambalo ni shilingi milioni nane lakini nne na elfu hamsini ili mradi uanze kufanya kazi" Chritopher Luahgila, Katibu Itikadi na Ueneze Mkoa wa Mbeya