Jumamosi , 15th Jan , 2022

Takwimu za matokeo ya mtihani wa kidato cha nne zinaonesha kuwa watahiniwa wa kidato cha nne hawakufanya vizuri katika mtihani wa taifa kwa somo moja la Hesabu.

Dkt. Charles Msonde, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA),

Kauli  hiyo imetolewa leo Januari 15, 2022, na Dkt. Charles Msonde Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), jijini Dar es Salaam, na kusema kuwa ufaulu wa kidato cha nne umeongezeka kwa kwa asilimia 1.46 ikilinganishwa na mwaka 2020.

“Takwimu za matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne zinaonesha kuwa watahiniwa wamefanya vizuri katika masomo mengi ya msingi ambapo ufaulu wa masomo hayo uko juu ya wastani kati ya asilimia 55.33 na watahiniwa hawakufanya vizuri katika somo moja la Basic Mathematics, ambapo ufaulu wa somo hili upo chini ya wastani," amesema Dkt. Msonde.