Jumatatu , 29th Feb , 2016

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Charles Kitwanga amesema vyombo vya usalama nchini vimefanya tafiti na kubaini vituo 86 maarufu kama matobo sehemu ambazo raia wanazitumia kutoroka kwenda nje ya nchi na kuingia ndani ya nchi.

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Charles Kitwanga

Waziri Kitwanga ameyasema hayo leo wakati akitoa ufafanuzi wa namna wizara hiyo ilivyoboresha usalama wa nchi hasa maeneo ya mipakani ambapo ndio maeneo ambayo wahamiaji wengi haramu wanapita kuingia nchini.

Aidha Waziri huyo wa Mambo ya ndani amesema kwakuzingatia usalama wa Raia ofisi yake imeagiza askari nchini kufanya uchunguzi zaidi kwa kila mkoa kufichua na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika na kujihusisha na vitendo vya kuwahifadhi wahamiaji haramu nchini na kuwasafirisha

Tanzania kwa sasa ina jumla ya wakimbizi takribani laki 2 na elfu 18 na mia sita kutoka nchi mbalimbali zikiwemo Burundi, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).