Jumanne , 10th Jun , 2025

Serikali ya Marekani imetangaza kuongeza wanajeshi zaidi mitaani kupambana na waandamanji wanaipinga msako wa kuwakamata wahamiaji nchini huko

Gavana wa California amesema amearifiwa kuwa wanajeshi elfu mbili zaidi watatumwa mjini Los Angeles kufuatia siku kadhaa za makabiliano kati ya waandamanaji na maafisa wa usalama kuhusu misako ya kuwakamata wahamiaji
Msemaji mkuu wa Ikulu ya Marekani Sean Parnell amethibitisha kuwa walinzi wengine wanapelekwa mjini humo.

Kwa agizo la Rais, Idara ya Ulinzi inakusanya Walinzi wa Kitaifa wa ziada 2,000 wa California kuitwa katika huduma ya usalama ya taifa kuwezesha maafisa wa kutekeleza sheria kwa ajili ya udumishaji usalama

Katika ujumbe kwenye mtandao wa X, Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance amesisitiza kutumwa kwa wanajeshi kukabiliana na maandamano ya kupinga uvamizi wa wahamiaji huko LA.

Hata hivyo Gavana Gavin Newsom ameitaja hatua hiyo ya Trump kuwa ni kutimiza ndoto ya rais dikteta huku mwanasheria mkuu wa California akimshitaki Rais Trump kwa kutuma majeshi jimboni humo bila ya ridhaa ya Gavana.

Waandamanaji wanaopinga kukamatwa kwa wahamiaji wamekusanyika Los Angeles kwa siku ya nne mfululizo. Polisi imesema waandamanaji wanaweka vizuiwizi kwenye barabara kadhaa, na ikatangaza kuzifunga baadhi ya barabara

Hii inajiri baada ya serikali ya Rais Donald Trump kuamuru kupelekwa kwa karibu wanajeshi 700 wa kitengo maalum kusaidia kupambana na machafuko yanayoendelea mjini humo.