
Austin ametangaza hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kundi la Ulinzi wa Ukraine linaloongozwa na Marekani akisema msaada huo unajumuisha mifumo ya kujilinda angani, makombora ya masafa marefu na maroketi na vifaa vya kuzuia mashambulizi ya droni ya Urusi.
Katika mkutano huo unaofanyika mjini Brussels, wanachama kadhaa wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, wameahidi kuendelea kuiunga mkono Ukraine katika vita vyake na Urusi.