Jumatatu , 22nd Feb , 2016

Marekani imesema imeona dosari kadha wa kadha katika chaguzi za Urais na Bunge nchini Uganda na kuongeza kuwa watu wa Uganda wanastahili mambo bora zaidi.

Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni

Tume ya uchaguzi ya Uganda hapo jana ilimtangaza Rais Yoweri Kaguta Museveni mshindi wa uchaguzi wa urais.

Museveni mwenye umri wa miaka 71 ambaye ameiongoza Uganda tangu 1986, atahudumu kwa muhula wa tano wa miaka mitano ijayo baada ya kutangazwa kushinda uchaguzi huo kwa zaidi asilimia 60.

Hata hivyo mpinzani wake wa karibu Kizza Besigye ambaye yuko katika kifungo cha nyumbani ameutaja uchaguzi huo kuwa bandia.