Jumatatu , 28th Apr , 2014

Maandalizi  ya  mkutano  wa  wakuu  wa  nchi  za  Jumuiya  ya  Afrika  Mashariki  unaotarajiwa  kufanyika  jijini   Arusha  siku ya  Tarehe  30/04/2014  yamekamilika 

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, samwel Sitta

Maandalizi  ya  mkutano  wa  wakuu  wa  nchi  za  Jumuiya  ya  Afrika  Mashariki  unaotarajiwa  kufanyika  jijini   Arusha  siku ya  Tarehe  30/04/2014  yamekamilika  ambapo     marais  wa  nchi  zote  Tano  wanatarajiwa  kupokea  mapendekezo  mbalimbali  ya    baraza  la  mawaziri  wa  nchi  hizo.

Waziri  wa  ushirikiano  wa  Afrika  Mashariki  wa  Tanzania  Mh  Samweli  Sitta  ametaja  baadhi  ya  mapendekezo  yatakayowasilishwa  kwenye  kikao  hicho  kuwa  ni  pamoja  na  hatua  iliyofikiwa  katika  michakato  mbalimbali  inayoaendelea  ukiwemo  wa   uundwaji  wa  shirikisho  la  kisiasa.

Mh  Sitta  ameongeza pia kuwa  mapendekezo  juu  ya    maombi  ya  nchi ya  Sudani Kusini kujiunga  kwenye  Jumuiya  ya  Afrika  Mashariki  yatawasilishwa.

Awali  akizungumza  katika  hafla  ya  uzinduzi  wa  maktaba  ya  Jumuiya  ya  Afrika  Mashariki  iliyozinduliwa  na  mwenyekiti  wa  baraza  la  mawaziri  wa  Jumuiya  hiyo  Bi Phillis  Kandie,  Mh  Sitta  amesema  baada  ya  kupatikana  kwa  maktaba  ya  Jumuiya,  nyaraka   na  kumbukumbu  zilizoko  katika  maeneo  mbalimbali  ya  nchi  wanachama zinatarajiwa  kurejeshwa   kwenye  maktaba hiyo 

Naye  mwenyekiti   wa  baraza  hilo  Bi. Phills  Kandie  amesema  kupatikana  kwa  maktaba  hiyo  ni hatua  kubwa   kwa  Jumuiya  na     ina umuhimu  mkubwa  na  itasaidia  kurahisisha  utekelezaji   wa   masuala  mbalimbali   ya  maendeleo  ya    nchi  wanachama  Jumuiya