Jumatano , 4th Jul , 2018

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa leo Julai 04, 2018 anatarijiwa kufungua rasmi maonyesho ya 42 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam,(Sabasaba) katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere vilivyopo jijini humo.

Muonekano wa lango la kuingilia katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba) vilivyopo jijini Dar es Salaam

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara(TANTRADE), Edwin Rutageruka amesema kuwa uzinduzi huo hapo awali ulitakiwa kufanyika hapo jana lakini kutokana sababu zilizo nje ya uwezo wao wameahirisha mpaka hii leo.

Rutageruka amewataka wananchi na wageni mbalimbali kutoka nje ya nchi kuendelea kufika katika maonyesho hayo na kuangalia fursa mbalimbali zilizopo kwa ajili ya maendeleo.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa maonyesho hayo yanashirikisha kampuni za ndani 2959, taasisi za serikali 127, na kampuni toka nje ya nchi zaidi ya 30.