Jumapili , 15th Aug , 2021

Wakati dunia imekuwa ikihangaika kutafuta namna ya kuwanusuru watu dhidi ya janga la virusi vya corona lililoibuka mwishoni mwa mwaka 2019, ikiwemo kuwapatia chanjo, mawazo ya wengine yamekuwa yakitaka kujua kuhusu usalama wa chanjo zenyewe.

Mmoja ya mwananchi akipata chanjo ya Uviko 19.

Chanjo hizo ambazo zimetengenezwa katika mataifa mbalimbali duniani na kupewa majina tofauti, tayari hivi sasa zinatumika kuwakinga watu na athari za ya virusi hivyo, ambapo wataalamu wamekuwa wakieleza kuwa ni salama na zinaleta mafanikio.

Tanzania licha ya awali kusita kuingiza chanjo hizo, hadi pale itakapojiridhisha usalama wake, sasa nayo miongoni mwa nchi ambazo tayari zimeingiza chanjo ya corona baada ya kujiridhisha na kuanza kuwachanja watu wake, kwa makundi yaliyopewa kipaumbele na kisha sasa watu wote kwa ujumla.

HALI IKOJE TANZANIA BAADA YA KUPOKEA CHANJO

Wakati dunia imekuwa ikihangaika kutafuta namna ya kuwanusuru watu dhidi ya janga la virusi vya corona lililoibuka mwishoni mwa mwaka 2019, ikiwemo kuwapatia chanjo, mawazo ya wengine yamekuwa juu ya usalama wa chanjo zenyewe.

Chanjo hizo ambazo zimetengenezwa katika mataifa mbalimbali duniani na kupewa majina tofauti, tayari zimegunduliwa na hivi sasa zinatumika kuwakinga watu na athari za ya virusi hivyo.

Tanzania licha ya awali kusita kuingiza chanjo hizo, kwa sasa ni miongoni mwa nchi ambazo tayari zimeingiza chanjo ya corona kwa ajili ya kuanza kuwachanja watu wake, hasa kwa makundi yaliyopewa kipaumbele.

Hiyo ni baada ya kupokea awamu ya kwanza ya msaada wa dozi 1,058,400 za chanjo dhidi ya virusi vya corona kupitia mpango wa Covax facility kutoka Marekani na nyingine zikiwa zimepokewa upande wa Zanzibar.

Chanjo iliyoingia nchini aina ya Johnson& Johnson imetengenezwa na Janssen Vaccines, Leiden, Netherlands, Belgian parent company Janssen Pharmaceuticals, subsidiary of American company Johnson & Johnson na huchomwa mara moja kwa mhusika.

Rais Samia Suluhu Hassan ameshazindua utoaji wa chanjo hiyo nchini Julai 28 ambapo pia alichanjwa yeye pamoja na viongozi wengine.

Kabla na baada ya kuwasili kwa chanjo hiyo nchini, watu wamekuwa na hisia tofauti, huku baadhi wakieleza kutokuwa tayari kuchanja kutokana na kile wanachodai kuwa “hata ukichanjwa unapata maambukizi.”

KABLA YA KUCHANJWA

Kulingana na utaratibu uliweka hapa nchini, kabla ya mtu hajapatiwa chanjo atatakiwa kujaza fomu maalumu ya kukubali kupata chanjo hiyo na baada ya hapo huchanjwa.

Pia mhusika hutakiwa kuwa na kitambulisho kimojawapo kati ya kile ya taifa, cha mpiga kura au leseni ya udereva kwa kuwa waliochanjwa wanaingizwa kwenye kanzidata.

 

Mkurugenzi wa kuratibu na kukuza utafiti kutoka Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu, (NIMR) Dkt. Paul Kazyoba alisema kabla ya chanjo, ni muhimu mwili ukawa na sawa na wenye nguvu za kutosha. “Muda huo unaingiza kitu kipya mwilini, unaposhtuka na kuanza kupata uchovu na maudhi pale ndiyo unazalisha seli kinga kuuandaa mwili, ili adui akijaribu kuingia akutane na kinga muda huo. Mhusika akiona maudhi yanazidi amtafute daktari ingawa wanaopata hali hiyo ni wachache,” alisema

BAADA YA KUCHANJWA

Baada ya kuchanjwa mhusika hupewa kadi inayoonyesha kuwa umeshapatiwa chanjo dhidi ya ugonjwa huo. Baada ya mtu kupata chanjo miongoni mwa mambo ya kuzingatia yanayosisitizwa ni kutopata kilevi cha aina yoyote kwa saa 72 sawa na siku tatu.

Hiyo inatokana na kwamba pombe na dawa ya chanjo vyote vinakwenda kwenye ini, hivyo upo uwezekano wa ini kuongezewa mzigo na kulichosha.

Kwa mujibu wa Dkt. Paul Kazyoba alisema baada ya kuchanjamtu hatakiwi kutumia kilevi chochote, kwani kitaingilia mfumo wa uzalishaji wa kinga za mwili ambao unafanywa na chanjo kwa saa za mwanzo.

Dk Kazyoba alisema chanjo inapochomwa mwilini, ikiingia inaenda kuzisisimua seli za kinga ‘antibodies’ na zinazalishwa na zikishajaa mwilini zinakuwa askari wa kupambana na kirusi kitakachoingia.

“Kuufanya mwili uzalishe hizi seli kinga, inatakiwa usiingiliwe na kitu chochote cha tofauti kwenye damu kwa saa 72. Kilevi cha aina yoyote kwa maana ya pombe, bangi, shisha au dawa za kulevya lazima kitaingilia mfumo na hivyo kuifanya chanjo kutofanya kazi yake vizuri.

Kati ya mambo ya kuzingatia baada ya kuchoma chanjo, inatakiwa mtu aushughulishe mwili kwa kipindi cha saa 72 za awali kwani kwa kufanya hivyo seli za kinga huzalishwa kwa wingi na huwa na manufaa zaidi tofauti na kinyume chake.

ATHARI (MAUDHI) ZA CHANJO

Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, baada ya mtu kuchanjwa anaweza kupata athari (maudhi) ndogo kama kuhisi kichefuchefu, kichwa kuuma, kupata uchovu kidogo na homa kwa mbali.

Mtaalamu wa macrobaiolojia kutoka Chuo Kiku cha Afya Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Dkt. Mtebe Majigo alisema mtu anapopewa chanjo yoyote anaweza kupata maudhi madogo madogo kama homa, ingawa si wote.

“Wakati mwili unapozalisha vichocheo vyake ambavyo ndiyo vitakuwa kinga ya mwili, vichocheo vingine ndiyo vinasababisha homa kutokea. Vinavyotoka ndiyo vinapeleka taarifa kwenye ubongo na vinarudi kama homa, hii ni baada ya mwili kushtuka kutokana na kilichoingia, lakini hali hii inatofautiana kati ya mtu na mtu,” alisema Dk Majigo.

Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk Tigest Mengestu alipozungumza siku ya kupokea awamu ya kwanza ya chanjo zilizoletwa nchini, alisema kupata chanjo ni miongoni mwa njia za kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona, lakini haiondoi au kuweka ukomo wa matumizi ya njia nyingine za kujikinga dhidi ya ugonjwa huo.

USALAMA WA CHANJO YA CORONA

Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Profesa Yunus Mgaya alisema usalama wa chanjo dhidi ya Covid-19 ni asilimia 99.9 na akawataka wananchi kuondokana na hofu.

“WHO haipitishi dawa kirahisi, ina kamati zake na imethibitisha chanjo zote aina sita ni salama na hapa Tanzania pia chanjo hizo zinahakikiwa kitaifa na taasisi zinazoshughulika na masuala ya afya.

“Sina wasiwasi na hii chanjo, na ikianza kutolewa mimi nitakuwa kati ya watu watano wa mwanzo,” alisema mtaalamu huyo.

 

WANANCHI WALIOCHANJA WANASEMAJE?

Estabella George ni mmoja wa Watanzania waliopata chanjo hiyo anaeleza kuwa, baada ya kuchanja alirudi nyumbani akiwa sawa, lakini baadaye alihisi maumivu ya kichwa na kuingiwa na hofu hali iliyopelekea kumtafuta daktari wake.

“Nilichoma chanjo asubuhi lakini baadaye usiku nilianza kuhisi maumivu ya kichwa ndipo nilipoamua kumtafuta daktari na baadae alinielekeza kunywa maji mengi na kupumzika hiyo ni hali ya kawaida, japo nilikuwa mwenye hofu kutokana na maneno ya mitandaoni kuwa chanjo hii sio salama”, alisema Estabela.

Aisha Yassin ni mkazi wa Dar es Salaam yeye ana mawazo tofauti kuhusu chanjo ya Johnson&Johnson akitaka serikali itoe elimu ya kutosha ili kusaidia Wananchi huku akisisitiza yeye hawezi kuchoma chanjo.

“Mtaani tunaambiwa maneno mengi tunavurugwa nani anasema ukweli kuhusu chanjo kwakweli mimi naogopa siwezi choma chanjo nasubiria kwanza nione wenzangu waliochoma”, anasema Aisha

MAMA ANAYENYONYESHA ANARUHUSIWA KUPATA CHANJO?

Swali hili linajibiwa na Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya Tiba ya  Chuo Kikuu  cha Afya na Sayansi ShirikishiMuhimbili (MUHAS) Dkt. Grace Shayo anasema hakuna madhara yoyote ya kiafya kwa mtoto endapo mama anayenyonyesha atapata chanjo ya Uviko-19.

Shayo ambaye ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani ya Mapafu na Maambukizi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili anasema mama anaponyonyesha mtoto baada ya kupata chanjo inafanya na mtoto kuogeza kingamwili na kuepuka magonjwa.”

“Baada ya mama kuchoma chanjo kinachopatikana kwenye maziwa yake ni zile kingamwili ambazo zimezalishwa na chanjo inayotengenezwa na mwili na sio chanjo ndo maana kwenye unyonyeshaji ndo maana tunasisitiza  wanyonyesha watoto.

“Na Kwasababu maziwaya mama ni kinga kwa mtoto kupata mgonjwa mbalimbali Chanjo zitakapotengeza kinga ambayo ni ‘antibody ‘ itapitaa kwenye maziwa ya mama na maziwa ya mama yatamkinga mtoto na maambukiziyaUviko -19 baada ya kupata chanjo kupatia maziwa,”anaeleza Dkt. Shayo.

ELIMU SAHIHI KUHUSU CHANJO TANZANIA

Kauli za wale wanaoipinga chanjo zinanadai kuwa, chanjo hiyo inabadili mfumo wa vinasaba vya mtu jambo ambalo limekatazwa katika baadhi ya iman za dini, lakini hoja za wengine zisizojiegemeza kwenye imani zinasema huu ni mpango wa mataifa tajiri katika kupunguza idadi ya watu ulimwenguni, jambo ambalo limepingwa vikali kupitia machapisho ya kisayansi na maandiko ya kidini.

 

Kauli za baadhi ya viongozi wa dini zinaonesha imani kubwa iliojaa ushawishi na utayari kwamba watainadi chanjo kwani ni sehemu ya tiba ambayo imethibitishwa na wanasayansi katika kukabiliana na janga la corona ambalo limegharimu maisha ya watu zaidi ya milioni tatu ulimwenguni na kuyaacha mataifa yakiwa kwenye tafakuri pana katika kujinasua kwenye janga hilo.

Baadhi ya viongozi wa dini nchini Tanzania wamesema watabeba jukumu la kueleza umuhimu wa chanjo ya Covid-19 katika dunia ya sasa inayokabiliwa na janga hilo hatari lililogharimu masiaha ya mamilioni ya watu ulimwenguni.