Jumatano , 9th Dec , 2015

Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuboresha upatikanaji wa huduma muhimu za afya na elimu kwa haraka.

Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania The.Samia Suluhu Hassan akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam walipofanya zoezi la Usafi

Akizungumza mara baada ya kushiri kufanya usafi katika kuadhimisha siku ya uhuru wa Tanzania Bara kama ilivyoagizwa na Rais wa Tanzania, Mhe.Suluhu amesema wananchi wajenge tabia ya kufanya usafi kwa hiari ili kuondokana na magonjwa yanayoweza kuzuilika.

Aidha Mh. Samia Suluhu Hassan amewapongeza waliojitokeza katika zoezi hilo na kuwataka wananchi waendelee na zoezi hilo sio mpaka siku ya Uhuru, ili kuwasaidia wananchi kuondokana na ujinga pamoja na maradhi yanayowakabili ikiwa ni pamoja na magonjwa ya mlipuko kama Kipindupindu.

Mh. Samia ameongeza kuwa tangu nchi inapata uhuru ilikuwa na kauli mbiu ya Uhuru na Kazi kwa hiyo Watanzania hawana bundi kudumisha utamaduni wa kuwa wachapa kazi ili kuliendeleza taifa la Tanzania.

Amesema serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuboresha upatikanaji wa huduma muhimu za afya na elimu kwa haraka, ili kuwasaidia wananchi kuondokana na ujinga pamoja na maradhi yanayowakabili ikiwa ni pamoja na magonjwa ya mlipuko kama Kipindupindu.

Mhe.Suluhu amesema wananchi wajenge Tabia ya kufanya usafi kwa hiari ili kuondokana na magonjwa yanayoweza kuzuilika.