Watoto waliouawa kikatili baada ya kufukiwa kutoka kwenye shimo
Watoto hao wamefukiwa katika nyumba walimo kuwa wakiishi iliyoko katika mtaa wa Salmini kata ya Chemchemu manispaa ya Tabora
Wakizungumzia tukio hilo linalodhaniwa kutokea kuanzia asubuhi ya terehe 25/01/2015, hadi walipogundua tukio hilo usiku za saa moja, mwenyekiti wa mtaa wa Barehani pamoja na wananchi walioshuhudia tukio hilo usiku, amesema kuwa watoto hao hawakuonekana wakicheza kama mazoea yao,
Aidha Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Tabora kamishna msaidizi Juma Bwire, pamoja na matukio kadhaa yaliyotokea, Jeshi la polisi linasikitishwa na tukio hilo la kikatili, ambapo amesema upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.
Amewataja marehemu kwa majina kuwa ni Mwamvua Mrisho (miaka 4) na Soud, ( miezi 4).