Jumanne , 23rd Oct , 2018

Kufuatia Mkoa wa Dar es salaam kuibuka kinara kitaifa katika matokeo ya mitihani ya darasa la saba yaliyotangazwa leo na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameibuka na kuwapongeza watumishi wa elimu Dar es salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Makonda ameandika, “nawapongeza sana sana walimu, waratibu kata, maafisa elimu , wazazi pamoja na wanafunzi kwa kuunganisha nguvu na hatimaye tumeongoza katika matokeo ya darasa la saba Tanzania."

Makonda ameendelea kusema, “asanteni sana kwakunivisha nguo na kumpa heshima Rais wetu mpendwa. Ofisi yangu itaandaa utaratibu wa kutoa zawadi kama motisha na asante kwa kazi wanayoifanya walimu pamoja na wanafunzi. Tumeongoza tena kwa mara nyingine tena.”

Katika matokeo yaliyotangazwa leo na NECTA kupitia Katibu Mtendaji wa Charles Msonde aliitaja Dar es salaam kuibuka kinara kitaifa ikifuatiwa na Mkoa wa Geita na Mkoa wa tatu ukiwa Arusha.

Jumla ya watahiniwa 733,103 kati ya 943,318 wamefaulu mtihani huo wa kuhitimu elimu ya msingi uliofanyika septemba 5 na 6 mwaka huu sawa na asilimia 77.72 kati yao wasichana 382, 273 na wavulana 350,273