Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango,
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, Mjini Dodoma, amesema kuwa TCRA, inatakiwa kuhakikisha kuwa makampuni ndio yanayolipa makato hayo kutoka kila tozo ya pande zote zinazotumia miamala hiyo ya utoaji na utumaji fedha kwa njia ya simu.
Dkt. Mpango amesema kuwa makampuni hayo yamekuwa yakipata faida kubwa kutokana na huduma zao lakini hawalipo kodi inavyotakikana hivyo watahikikisha makampuni hayo ndio yatakayobeba mzigo huo wa ulipaji kodi bila kuathiri makato ya awali kwa wateja wao.
Amesema sheria inavyotaka ni kuwa ada ambayo inakatwa katika utumaji au upokeaji wa mialamala hiyo ya fedha ndio inayotakiwa kukatwa kodi na sio kuongeza ada zaidi kwa ajili ya kulipia hizo asilimia 10 na kusema jambo hilo lingewaumiza wananchi.