Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Vijijini Bw. Wilman Ndile
Wanafunzi hao wametoa ombi hilo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Abdulrahman Kinana, ambapo wamesema kuwa ofisi hizo kuwa jijini Dar es Salaam na sehemu nyingine nchini hakutoi fursa kamili kwa mashirika na makampuni hayo kukuza kikamilifu uchumi wa mikoa hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Vvijijini Bw. Wilman Ndile amesema kuwa, kwa sasa sehemu kubwa ya ulipaji kodi mbalimbali za makampuni hayo yamekuwa yakilipiwa Jijini Dar es Salaam, na kusema hali hiyo imekuwa ikikosa mabilioni ya shilingi zitokanazo na ulipaji kodi.
Akiwa katika mji wa Mtwara, Kinana, alikagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kushiriki ujenzi, sanjali na ukaguzi wa majengo ya chama hicho yaliyochomwa moto kwenye vurugu za gesi katika mkoa huo, na kutembelea mtaro wa kutililisha maji ya mvua katika mji wa Mtwara kwenda baharini...