Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam Dkt. Valentino Mokiwa.
Hayo yamesemwa leo katika ibada ya Pasaka iliyoadhimishwa kitaifa Jijini Dar es Salaam, katika Kanisa la Mtakatifu Albano lililopo Upanga, na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam Dkt. Valentino Mokiwa.
Askofu Mokiwa amesema kuwa imefika wakati sasa makanisa yajitathmini yenyewe na kuanza kupunguza kuzungumza mambo ya nje ya kijamii na badala yake waelekezane uovu unaopatikana ndani ya Makanisa.
Aidha Askofu Mokiwa ameongeza kuwa makanisa yaache mashindano ya umiliki wa taasisi za kijamii, kushutumiana na kujengeana chuki baina yao, tamaa za madaraka pamoja na ubadhirifu wa mali za kanisa na kusema hayo ni kati ya majipu yanatotakiwa kutumbuliwa ndani ya makanisa.
Askofu Mokiwa amesema kuwa jambo lingine ambalo linashusha hadhi ya makanisa ni pamoja na kuwepo na mgawanyiko wa makundi tofauti tofauti hali inayopeleka kanisa kukosa nidhamu na kuheshimika.
Pia Askofu Mokiwa ameonya kuhusu uwepo wa kile alichokiita "Injili za Kibiashara" ambapo baadhi ya makanisa hutumia injili kwa ajili ya kujiingizia kipato kwa kufanya miaujiza.
Msikilize hapa wakati akitoa ujumbe wake katika ibada ya Pasaka:-