Jumanne , 6th Sep , 2016

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt. Binilith Mahenge amesema upatikanaji wa maji kwa baadhi ya maeneo katika mkoa huo bado ni wa kusuasua kutokana na kutokuwepo kwa miundombinu rafiki ya ujenzi wa huduma hiyo,

kuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt. Binilith Mahenge.

Kufuatia hali hiyo amesema hadi sasa tayari ofisi yake imeanza kufanya uchunguzi wa maeneo ambayo hayafikiwi na huduma ya maji kabisa.

Dkt. Mahenge ameyasema hayo kwenye mahojiano maalum na East Africa, na kuongeza kuwa tayari ameagiza viongozi wa vijiji kuorodhesha maeneo ambayo hayafikiwi na huduma hiyo ili serikali itafute njia mbadala zakufanya kuwezesha maeneo hayo kupata maji safi na salama kwa ajili ya matumizi yao kila siku.

Amesema baadhi ya maeneo ambayo yatanufaika na mradi huo wa maji ambao unaotarajiwa kuwekwa ni pamoja na maeneo ya zahanati, mashuleni, ofisi mbalimbali za serikali na sehemu ambazo zinatoa huduma kwa jamii bila ubaguzi wa itikadi zao, kwakuwa serikali ya awamu ya tano ina lengo la kuwahudumia watanzania wote.

Kwa upande wa afya Dkt. Mahenge amesema katika awamu hii ameagiza viongozi wa mkoa huo kujenga zahanati moja kila mwaka kwenye kata zote zilizopo katika mkoa wa Ruvuma na kuziagiza halmashauri kupeleka fedha kwenye vijiji ambavyo vimepangiwa kujenga Zahanati hizo kwa wakati uliowekwa na serikali.