Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makalla amethibitisha ujio wa Waziri Mkuu mkoani humo,alipotembelea ofisi za makao makuu ya Tajati leo (Julai 13) na kuzungumza na wanachama.
Makalla amesema waziri mkuu, atafanya uzinduzi wa chama hicho wakati wa ziara yake ya kufunga maonesho ya wakulima ya Nanenane Kanda ya Nyanda za Juu Kusini mwaka 2016 yatakayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Wakati huo huo mkuu huyo wa mkoa amekitaka chama hicho kuwa na mtazamo wa mbali zaidi kwa uongozi kuanza mikakati ya kuanzisha chombo kingine kikubwa cha kibiashara kitakachounganisha fursa za uwekezaji na utalii na zile zilizopo kwenye mataifa yaliyoendelea.
Amesema upo uwezekano wa Tajati kuwa na taasisi nyingine ya kibiashara ikiwepo ya kupokea na kuwaongoza watalii ili iweze kujiingizia fedha na kujiendesha badala ya wanachama kuishia kuandia na kutangaza utalii pekee.
Aidha, Makalla ameahidi kuendelea kushirikiana na Tajati kama ilivyo kwa viongozi wengine ambao tayari wametembelea ofisi za chama hicho kbla yake.




