Ijumaa , 1st Apr , 2016

Mahakama ya juu nchini Uganda jana imetupilia mbali shauri lililokuwa linapinga kuchaguliwa tena kwa rais Yoweri Museveni, mwezi Februari, na kusema mchakato huo ulikuwa wa haki na wa wazi.

Jaji Mkuu wa Uganda, Bart Katureebe

Shauri hilo liliwasilishwa na mgombea wa upinzani Amama Mbabazi, ambaye alitoa hoja za kucheleweshwa kwa vifaa vya kupigia kura, vitisho na kukamatwa kwa viongozi wa upinzani.

Shauri hilo pia linadai kuwepo na ushahidi wa udanganyifu, ikiwa ni pamoja na kupiga kura mara nyingi, na kuundwa kwa vituo haramu vya kupigia kura Februari 18.

Jaji Mkuu wa Uganda, Bart Katureebe alikataa pingamizi hilo, akisema hakukuwa na ushahidi ulioonyesha ushindi wa rais Museveni ulikuwa wa udanganyifu. Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 71 alimeitawala nchi hiyo ya Uganda tangu 1986, alitangazwa mshindi kwa kupata asilimia karibu 61 ya kura.