Alhamisi , 23rd Jun , 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ameipongeza tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), kwa kusimamia zoezi la Uchaguzi vizuri na kuahidi kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo kuwa na jengo lao binafsi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,akiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam, wakati akikabidhiwa ripoti ya Uchaguzi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), Dkt. Magufuli amesema kuwa atatoa shilingi bilioni 12 kwa ajili ya ujenzi wa majengo hayo ambapo amependekeza yajengwe Mkoani Dodoma.

Dkt. Magufuli amesema kuwa tume hiyo imefanya kazi kubwa licha ya kuwa na upungufu wa bajeti wa kununua vifaa vya uandikishaji lakini pia ufinyu wa maadalizi lakini waliweza kufanikisha kuandikisha kwa wakati zoezi la upigaji zima la uchaguzi kwa nchi nzima.

Aidha rais Magufuli amesema kwa moja ya changamoto zilizomgusa ni pamoja na Tume kukaa katika jengo la kupanga wakati kutokana na ufinyu wa kazi zake tume haitawiki kukaa katika jengo hilo hivyo amerudisha bakaa aliyopewa na tume ili iweze kujenga majengo ya Tume.

Aidha Rais Magufuli amesema kuwa licha ya zoezi hilo kukamilika lakini tume inahitaji kuendelea na shughuli zake za kawaida ikiwemo kuboresha daftari la kudumu la wipiga kura pamoja na utoaji wa elimu ya mpiga kura na kusimamia chaguzi ndogondogo.

Sauti ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,