Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,
Akizungumza jana wakati alipotembelea kanisa linaloongozwa na Mchungaji Anthony Lusekelo lililopo Ubungo Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema kuwa atahikikisha sera yake ya hapa kazi tu inatekelezeka kwa vitendo zaidi.
Rais Magufuli amesema kubwa ambalo anaendelea kuliomba ni kwa Watanzania wote bila kujali itikadi zao na imani zao kuendelea kuiombea serikali ya awamu ya tano ili iweze kutekeleza ahadi walizozitoa wakati wa Kampeni.
Rais Magufuli ambae alifanya ziara ya Ghafla katika kanisa hilo alitoa ahdi ya ujenzi wa barabara ya Ubgungo Kibangu hadi Liverside ili kuwaondolea adha waumini wa kanisa hilo na wananchi wa ubungo kibangu ambayo wanaipata kupita barabara hiyo.