
Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi, Benjamin Kuzaga.
Familia hiyo ilipotea miezi miwili iliyopita huku ndugu jamaa na marafiki kwa kushirikiana na mamlaka husika, walifanya jitihada za kuwatafuta bila mafanikio jambo ambalo lilileta hofu kubwa kwa wakazi wa kijiji hicho.
Wananchi waliendelea kufanya uchunguzi na kuikuta miili hiyo mlimani na waliweza kuzitambua nguo za marehemu ambazo walikuwa wakizivaa wakati wa uhai wao .
Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi Benjamini Kuzaga, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini watu waliohusika na mauaji hayo ya kikatili.