Jumatano , 13th Apr , 2022

Shughuli za upakuaji mizigo za meli zimesitishwa katika bandari yenye harakati na shughuli nyingi nchini Afrika Kusini kufuatia mafuriko yaliyotokea katika jimbo la KwaZulu-Natal na kusababisha vifo vya watu takribani 59  .

Mafuriko hayo yameharibu miundombinu ya barabara , madaraja na makazi ya watu kufuatia mvua kubwa iliyonyesha siku tatu mfululizo.  

Bandari ya Durban imefungwa mpaka hapo itakapotolewa taarifa nyingine kutokana na uharibifu mkubwa uliotokea sababu ya mafuriko hayo 

Jiji la Durban limekua kitovu cha majanga ya asili nchini humo na kusababisha madhila kwa watu waishio maeneo hayo.  

Miundombinu ya mawasiliano na yenyewe imeharibiwa huku makampuni makubwa mawili ya simu yakiripoti kuwa zaidi ya minara 900 imeanguka.  Rais wa Afrika kusini  Cyril Ramaphosa amekatiza ziara yake nchini Msumbuji ili kwenda kutembelea maeneo yaliyoathiriwa.  

Rais Ramaphosa atatathimini na kuangalia uwezekano wa serikali kuingilia kati huku akiziomba taasisi nyingine kuzisadia jamii zilizoathiriwa na mafuriko hayo.  

“hili ni tukio kubwa sana la asili ambalo linatulazimu serikali kuingilia kati  ," amesema Rais Ramaphosa. Kumekua na ripoti ya makontena ya mizigo ambayo yamsombwa na mafuriko na kupelekwa mpaka barabara kuu za nchi hiyo