Jumatatu , 18th Apr , 2016

Mbunge wa Mtwara Mjini kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maftaha Nachuma, amepingana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) juu ya mikoa ya Mtwara na Lindi kuwepo katika mradi wa kusambaza gesi majumbani kutekelezwa na shirika hilo.

Mbunge wa Mtwara mjini kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maftaha Nachuma

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kuwapongeza wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge ulioambatana na zoezi la kutambulisha magari ya kubebea wanafunzi katika uwanja wa Mashujaa , Nachuma amesema amepitia mpango wa shirika hilo na kujiridhisha kuwa mikoa hiyo haipo katika mradi huo.

Hata hivyo, kauli hiyo ya Mbunge huyo inapingana na maelezo yaliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, James Mataragio, ambayo alimweleza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, alipofanya ziara katika kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Madimba mkoani Mtwara Februari 27 mwaka huu.

Mbali na maelezo hayo yaMmkurugenzi, Meneja wa Biashara ya Gesi wa TPDC, Emmanuel Gilbert, aliwahi kuwaeleza waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa semina ya siku moja kwa waandishi juu ya kuwajengea uwezo wa masuala ya mafuta na gesi, kuwa shirika lipo katika mchakato wa ujenzi wa mradi huo na kwamba tayari upembuzi yakinifu katika mikoa ya Lindi na Mtwara umekamilika.

Sauti ya Mbunge wa Mtwara mjini,Chama cha Wananchi (CUF), Maftaha Nachuma,