Uongozi wa kata ya Mang’oto wilayani Makete mkoani Njombe umeamua kuweka utaratibu wa kuwasajili madalali wote wa viazi katika kata hiyo ili kuepuka changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wakulima ikiwemo kutapeliwa
Hayo yamejiri kwenye mkutano uliowakutanisha wakulima na madalali wanaonunua viazi katika kata hiyo Januari 24, 2025 ambapo utaratibu huo utaanza kutumika mara moja sanjari na kuwa na ujazo unaofaa wa gunia la viazi
Osmund Idawa diwani wa kata ya Mang’oto na Augustino Ngailo Afisa Tarafa ya Lupalilo kwa pamoja wameeleza sababu za kuitisha mkutano huo kuwa ni pamoja na kudhibiti utapeli unaofanywa na madalali wasio waaminifu pamoja na wakulima wenye tamaa wanaowatapeli madalali
Baadhi ya madalali wameelezea namna wanavyofanya kazi hiyo na kukubali kusajiliwa ili watambulike huku wakiomba kuongezewa muda mpaka Jumatatu Januari 27, 2025 wawe wamechukua viazi ambavyo wameshavifunga kwa ujazo Zaidi (rumbesa) na baada ya hapo utaratibu waliokubaliana uanze kutumika Kwa upande wao wakulima wa viazi wamesema wanafurahishwa na utaratibu huo ambao utawasaidia kuwabaini madalali wasiofaa huku wakishauri wale ambao wamekuwa wababaishaji wasiruhusiwe kufanya kazi hiyo.