Jumapili , 11th Nov , 2018

Katibu Mkuu wa chama cha CUF Maalim Seif Sharif Hamad amemwomba Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kutolea ufumbuzi wa mapungufu ya kikatiba na sheria juu ya suala la usimamizi wa uchimbaji wa mafuta na gesi kwa upande wa Zanzibar.

Katibu Mkuu wa chama cha CUF Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa na Rais Magufuli.

Katibu Mkuu wa chama cha CUF Maalim Seif Sharif ahamad amemwomba Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kutolea ufumbuzi wa mapungufu ya kikatiba na sheria juu ya suala la usimamizi wa uchimbaji wa mafuta na gesi kwa upande wa Zanzibar.

Akiongea na waandishi wa habari leo kufuatia utiaji saini wa mkataba wa ugawaji faida PSA baina ya Zanzibar na kampuni ya RAK GAS, kampuni ambayo itaendesha shuguli za uchimbaji wa mafuta na gesi Zanzibar, Maalim Seif amesema mkataba huo ni batili kwani kuna mkinzano mkubwa wa kisheria na kikatiba ambao amesema usipo shugulikiwa hivi sasa ufumbuzi wake utakuwa mgumu kwasiku za baadae.

"Kwavipengele hivyo, sheria zilizotungwa na Zanzibar kuusiana na masuala ya mafuta na gesi nibatili  mgongano wa kikatiba na ule wa kisheria kwa pamoja unaathari kubwa sana kwani sheria ya mafuta na gesi 2015 ya Tanzania imeeleza bayana nani nimmiliki wa mafuta na gesi," amesema Maalim Seif.

Maalim Seif ametaja mapungufu ya kikatiba kuwa nipamoja na kwamba Suala la Mafuta na Gesi, katiba ya Jamuhuri ya Muungano imelitaja kama suala la Muungano na sio suala la Zanzibar, na kwamba amesema ibara ya 64 kipengele 3 ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano was Tanzania inabatilisha Sheri iliyotungwa na baraza la wawakilishi kwa jambo ambalo ni la Muungano ni batili.

Oktoba 23, 2018 wakati hafla ya utiaji saini mkataba huo Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein alisema mchakato huo umezingatia sheria zote za Zanzibar na si vinginevyo.