Ijumaa , 29th Mei , 2015

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema afya yake ni nzuri na yupo imara kuwaongoza Wananchi wa Zanzibari akiwa kama rais wao hii ni baada ya hapo jana kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo kwa upande wa Visiwani.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad

Maalim Seif amesema hayo jana wakati akichukua fomu hiyo katika ofisi za CUF, Bububu wilaya ya Magharibi kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba 25 mwaka huu.

Amesema hakuna atakemzuia kuwa rais wa Zanzibar na kuwataka wafuasi wa chama hicho kuwa na mshikamano ili kuibuka na ushindi katika uchaguzi huo.

Aidha Maalim Seif ametaja vipaumbele vyake pindi akiingia madarakani ikiwa ni pamoja kuwaboresha maisha wananchi wa Zanzibar pamoja kuhakikisha amani na mshikamano pamopja na haki sawa kwa watu wote bila upendeleo.