Ijumaa , 16th Mei , 2014

Mapendekezo ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Utouh, ya kuitaka Serikali kutowateua wabunge kuwa wajumbe wa bodi za mashirika ya Umma hayajatekelezwa kwa miaka mitatu mfululizo.

Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa serikali nchini Tanzania CAG Ludovick Utouh.

Ripoti ya CAG ya ukaguzi wa mashirika ya Umma kwa mwaka 2013/2014 iliyowasilishwa Bungeni mjini Dodoma imesema mapendekezo hayo yaliwasilishwa kwa mara ya kwanza 2008/2009.

Aidha CAG alisema kanuni za utawala bora zinahitaji watendaji wakuu wa mashirika ya Umma wateuliwa na bodi ya wakurugenzi wa mashirika hayo badala ya kazi hiyo kufanywa na Rais.