Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi mh. William Lukuvi.
Akizungumza na East Africa Radio leo jijini Dar es Salam Mh. Lukuvi amesema kuwa watendaji wengi wameokuwa wakifanya kazi kimazoea na kuongeza kuwa kuna watu wengine wenye nguvu ya hela wanavamia viwanja bila kufuata sheria na kusababisha migogoro.
Mh. Lukuvi amewataka maafisa ardhi katika kila wilaya kutengeneza dawati la ardhi ambalo kila wiki liwe linasikiliza kero za watu wenye migogoro ya ardhi na kuzitafutia ufumbuzi.
Amesema atawafukuza kazi na kuwafikisha mahakamani watendaji wote watakaokiuka maadili ya kazi na pia atawafikisha mahakamani wale wote wanaovamia viwanja kwa kutumia nguvu.
Mh. Luvuki amesema kuna watu ambao walivamia viwanja mmojawapo akiwa ni aliyevamia kiwanja cha mama Maria Nyerere na kujenga nyumba ambapo yeye mwenyewe kuivunja lakini kesho yake akaanza kujenga tena kwa nguvu akiwa chini ya usimamizi wa walinzi 21.