Jumanne , 12th Jul , 2016

Asilimia 70 ya watanzania hawatambui na hawajuai wapi pa kupata haki zao za msingi za kimaendeleo ikiwemo haki ya kisheria.

Takwimu hizo zimetolewa jijini Dar es salaam na shirika lisilo la kiserikali la kupambana na umasikini na kutetea haki za binadamu LPLIO katika mahojiano na East Africa Radio kuwa watanzania wengi wananyimwa haki zao kutokana na kutokuwa na elimu juu ya majukumu ya serikali

Mkurugenzi wa shirika hilo bwana Peter Isare amesema nivyema serikali ikahakikisha Kuwa wananchi wake Wanapata huduma bora za afya, makazi na uhakika wa chakula sambamba na upatikanaji wa mazingira wezeshi ya kiuchumi ili kuondokana na umasikini.

“Kila mwananchi anapaswa kuwa na bima ya afya, lakini uwezi kukutana na huduma hiyo kwenye hosptali zilizopo vijijini watu wanakosa haki zao za msingi kwa kutojua ninini hasa wanapaswa kudai, bima ya afya niyakila haki ya kila mwananchi” amesema Peter

Peter amesema, ili kuondoa changamoto hizo nivyema serikali ikazisaidia asasi zenye lengo la kupambana na umasikini na haki za binadamu kuwafikia wananchi wake hasa maeneo ya vijijini ambako asilimia kubwa ya huduma azijafikishwa.