Jumatatu , 29th Feb , 2016

Bondia Francis Cheka ambaye anashikilia Ubingwa wa Mabara wa WBF anatarajia kupanda ulingoni kupambana na bondia Alexander Bland kutoka nchini Colombia.

Mwakilishi wa WBF nchini Tanzania ambaye pia ni Rais wa Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania TPBO Yassin Abdallah Ustadh amesema, Bondia Cheka amerudi kwa kasi na kuna uwezekano akapanda zaidi katika viwango vya dunia baada ya kumpiga bondia Mserbia anayeishi Uingereza, Geard Ajetovic siku ya Jumamosi.

Ustadh amesema, hivi sasa ni wakati wa kufanya maandalizi ya nguvu kwani bondia ambaye anatazamiwa kupambana na Cheka yupo vizuri hivyo maandalizi mazuri yatasaidia Cheka kuendelea kujiwekea rekodi nzuri katika masumbwi.