
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kitengo cha habari na mawasiliano cha Chadema, mkutano huo ni sehemu ya ziara ya viongozi waandamizi wa chama na UKAWA kwa ujumla, ambao watakwenda maeneo mbalimbali nchi nzima kuwashukuru wananchi, walivyounga mkono upinzani na agenda nzima ya mabadiliko katika uchaguzi mkuu uliopita.
Taarifa hiyo imesema kuwa katika ziara hiyo ya Tanga, Ndugu Lowassa ataambatana na viongozi wengine waandamizi wa UKAWA, na kwamba wananchi wanastahili shukrani kwa imani yao kubwa ambayo ni ishara ya wazi kuwa matumaini yao kwa miaka mingine mitano yatasimamiwa na kuongozwa na upinzani imara kupitia UKAWA.
Ikumbukwe kuwa idadi ya wabunge wa upinzani imeongezeka, kutoakana na wananchi wengi kuonyesha kuwa na imani na vyama vya upinzani, ambapo wabunge hao wataunda serikali yao mbadala na kusimamia pamoja na kuongoza halmashauri zipatazo 34 nchi nzima, ikiwa moja ya misingi imara katika kupigania mabadiliko.