Lowassa ametoa msimamo huo mjini Zanzibar wakati akizungumza na waumini wa madhehebu ya KKKT katika kanisa la mwanakwerekwe wakati akishiriki ibada ya Krismas yeye na familia yake ambapo alisema hali ya amani inaonekana waziwazi kwa vile kanisa hilo halina ulinzi wa askari wa vikosi vya FFU hali inayoashiria amani ipo na itadumishwa tafauti na miaka ya nyuma hali ambayo pia iliungwa mkono na mchungaji kiongozi Philip Mvungi.
Katika kanisa lingine la Tanzania Asemblies of God lilioko Kariakoo mjini Zanzibar ambapo huko nako waumini hao waliungana na wenzao duniani kote kukumbuka siku ya kuzaliwa mkombozi Yesu Kristo ambapo mchungaji mkuu wa kanisa hilo Dickson naye amesisitiza amani iwepo nchini huku akishauri serikali na taasisi huska ziwawekee mazingira mazuri watanzania wakati wa kupiga kura ya katiba mpya na wananchi wasilazimishwe.
Katika kanisa kuu la Anglikana lililoko Mkunazini ambapo waumini wa madhehebu hayo waliungana pamoja na kumuombea Yesu Kristo kwa nguvu zote huku Padre Nuhu Justin Salanya wa kanisa hilo kongwe ameisifu serikali kwa kuweza kudhibiti hali ya fujo kwa kuimarisha taasisi za ulinzi.
Katika hatua nyengine Rais wa Jamhuri ya muungano Dr Jakaya Kikwete amekabidhi msaada wa chakula na mbuzi wawili kwa nyumba za wazee wanaoishi Welezo ikiwa ni zawadi ya krismas ambapo wazee hao kupitia sister Gema walimshukuru Kikwete kwa kuwajali wazee.