Ijumaa , 23rd Sep , 2022

Mitandao ya kijamii nchini Kenya imegubikwa na tukio la watu kusomba vifuko vya unga wa mahindi , baada ya lori lililokua limebeba bidhaa hizo kupata ajali ya kupinduka katika barabara kuu ya jijini Nairobi.

Watu wanaonekana wakikwapua unga huo kwa kutumia pikipiki zao na baiskeli. 

Hakuna chanzo maalumu cha ajali hiyo ambapo polisi hawakuwepo kwenye tukio.

 Mfumuko wa bei za bidhaa muhimu nchini humo haswa unga wa mahindi na vyakula vingine umekua juu sana kutomana na sababu za ndani ya nje ya nchi hiyo. 

Wiki iliyopita serikali ya nchi hiyo iliondoa ruzuku kwenye mafuta ya petrol na kupelekea bei ya mafuta kuwa juu mara dufu.