
Hayo ameyasema leo akiwa Hospitali nchini Kenya ambapo yupo kwa matibabu tangu mwezi Septemba 2017, alipojeruhiwa mkoani Dodoma kwa kushambuliwa na watu wasiojulikana.
''Siachi kukosoa Serikali hata siku moja, nitadai haki hadi mwisho wa maisha yangu, nimekuwa na tabia ya kudai haki tangu nikiwa mdogo nafanya hivyo ili kuokoa Taifa langu'', amesema Lissu.
Lissu ambaye ni Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) amejinadi kwamba, yupo katika hali nzuri, amepona majeraha yote kilichobaki kusimama na kutembea. Mbunge huyo wa Singida Mashariki amehoji vyombo vya dola kukaa kimya akiwemo Spika wa Bunge, Jaji Mkuu wa Tanzania pamoja na Mahakama.
''Nimeshangazwa kwanini hadi sasa Jaji Mkuu wa Tanzania kukaa kimya, Mahakama pamoja na Spika hawakutoa kauli wakati mimi ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania'',amesema.