Mtaalamu wa masuala ya uchumi ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF.
Aidha Prof.Lipumba amesema pia tatizo la misamaha ya kodi kwa kiasi kikubwa inalinyima taifa pato kubwa ambalo lingetumika kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
Katika hatua nyingine, Profesa Lipumba amependekeza kuwa mapato katika sekta ya gesi na mafuta yagawiwe kwa wananchi masikini wakiwemo wazee pamoja kurekebisha miundo mbinu.
Kwa mujibu wa Profesa Lipumba nchi nyingi zimekuwa zikiwapatia fedha wananchi kutokana na rasilimali zilizopo katika nchi husika na kuongeza kuwa utaratibu uliopo sasa hauwezi kumnufaisha mwananchi wa kawaida kwa kuwa hapati faida hiyo moja kwa moja na badala yake kuna urasimu katika ugawaji wa mapato ya rasimali hizo.