Alhamisi , 12th Oct , 2023

Rais wa Liberia  George Weah, , atakubali matokeo ya uchaguzi mkuu wa Jumanne, afisa kutoka chama chake amesema.

 

Jefferson Koijee, katibu mkuu wa chama tawala cha Muungano wa Mabadiliko ya Kidemokrasia, aliwaambia waandishi wa habari: "Mtu huyu amesema mara nyingi kwamba amani ya nchi hii iko juu yake mwenyewe."

Lakini Bw Koijee aliondoa uwezekano wa kushindwa kwa Weah, nyota wa zamani wa soka mwenye umri wa miaka 57.

Maafisa wa uchaguzi walisema kuwa idadi ya watu waliojitokeza katika uchaguzi wa nne wa Liberia ilikuwa kubwa.

Kura zinaendelea kuhesabiwa   tume ya uchaguzi itaanza kutoa matokeo baadae leo.

Bw Weah anatarajiwa kukabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa aliyekuwa makamu wa rais Joseph Boakai, 78, wa chama cha Unite. Boakai alikuwa naibu wa Ellen Johnson Sirleaf wakati alipokuwa rais.