Ijumaa , 15th Mei , 2015

Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania linaloelekea kumaliza muda wake limetajwa kugubikwa na k

Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania linaloelekea kumaliza muda wake limetajwa kugubikwa na kasoro nyingi zilizopelekea wananchi kukosa Imani na Bunge hilo na hivyo kupoteza sifa ya kuwa chombo cha uwakilishi wa wananchi.

Akizungumza na East Africa Radio mwanasheria Hamisi Mkindi kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kitengo cha ufuatiliaji Bunge na chaguzi mbalimbali, amezitaja kasoro hizo kuwa ni pamoja na lugha chafu za matusi zilizopelekea Bunge kupoteza heshima yake mbele ya jamii

Bw Mkindi ameongeza kuwa hali hiyo ya bunge kutawaliwa na itikadi za vyama inaondoa uwajibishwaji kwa viongozi wa serikali ambao wameshindwa kutekeleza ahadi za mipango ya maendeleo katika wizara zao.

Mkindi amesema Bunge linawajibu wa kuisimamia serikali ili kuweza kutimiza wajibu wake hivyo amewataka wananchi kujiandikisha katika Daftari la kudumu la mpiga kura ili kuwachagua viongozi makini katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu.