Jumatatu , 16th Mei , 2022

Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, amesema hawezi kutangaza kuwa nafasi 19 za wabunge wa Viti Maalum wa CHADEMA ziko wazi, hadi hapo Mahakama itakapotoa uamuzi kwani Bunge haliwezi kuingilia mchakato wa Mahakama.

Baadhi ya wabunge 19 waliofukuzwa uanachama na CHADEMA na kulia ni Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson

Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 16, 2022, Bungeni Dodoma, na kuthibitisha kupokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika, ya kumtaarifu kuhusu wabunge hao kutokuwa wanachama wa chama hicho.

Tazama video hapa chini