Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, katika maadhimisho ya siku ya sikoseli duniani, Mkuu wa programu za Wanawake na Maendeleo (WAMA) Bi.Sara Maongezi amesema takwimu hizo zinaifanya Tanzania kushika nafasi ya tano katika nchi zenye wagonjwa wa sikoseli duniani.
Bi. Maongezi amesema upo umuhimu wa elimu kutolewa ili kuhamasisha jamii katika kupima na kutambua ugonjwa wa sikoseli na kuachana na imani potofu ikiwemo kuwanyanyapaa waathirika na ugonjwa huo.