Jumatatu , 21st Mar , 2016

Kiwango cha Joto katika Mji wa Moshi Mkoani Kilimanjaro, kimezidi kuongezeka hadi kufikia nyuzi joto 36 kiwango ambacho hakijawahi kutokea kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Mnara wa saa ambao ndiyo kielelezo kikubwa cha mji wa Moshi

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa Mkoa huo wamesema ongezeko hilo la joto linawatia wasiwasi hali inayowafanya washindwe kufanya shughuli zao kwa ukamilifu hasa wakati wa mchana na jioni.

Wakati mamlaka ya hali ya hewa ikisema kuwa miezi ya March na septemba hukumbwa na hali ya jua kusogea zaidi na uso wa dunia hali inayosababisha ongezeko la joto katika miezi hiyo lakini wakazi wa mkoa huo wamesema hali ya joto kuongeza imeanza kwa miaka mitatu iliyopita sasa.

Wakazi hao wanaimani kuwa ongezeko hilo la joto limetokana na mabadiliko ya tabia nchi hivyo wameiomba serikali iongeze juhudi katika usimamizi wa uharibu wa mazingira na kuongeza kupanda miti zaidi ili kupambana na mabadiliko hayo ya tabia nchi.