Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Dk Jasmin Tiisekwa
Mji wa Dodoma ni mji wa shughuli za bunge ambapo hivi karibuni bunge linatarajiwa kuanza vikao vyake hivyo kufanya mji kuwa na watu wengi katika kipindi hiki.
Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Dk Jasmin Tiisekwa katika kikao cha kamati ya afya ya msingi iliyolazimika kukutana kwa dharura kuangalia hali ya ugonjwa huo amesema kuwa kasi ya ugonjwa huo imekuwa ni kubwa kwa sasa.
Kikao hicho kilijumuisha wadau mbalimbali wa afya ambapo mganga mkuu wa manispaa ya Dodoma James Charles amesema kuwa kwa sasa wamefungua kambi katika viwanja vya Nanenane katika banda la afya ambapo hivi sasa kuna wagonjwa 7
Naye afisa afya idara ya mazingira Athanas Bais amesema tatizo la kutokuzolewa kwa taka katika maeneo mbalimbali hasa katika masoko kutokana na kuwepo kwa vifaa chakavu hasa magari ambapo lipo moja tu la tangu mwaka 1980 kunachangia uwepo wa ugonjwa huo