Mwenyekiti wa kamati ya maziko ya mwanasiasa huyo, Omary Kimbau amesema Kingunge atazikwa saa tisa alasiri.
Aidha amesema kwamba leo Ijumaa Februari 2, 2018 kuwa utaratibu na mipango mingine inaendelea kufanyika nyumbani kwake.
Kingunge amefariki dunia leo alfajiri akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikuwa akiuguza majeraha baada ya kung'atwa na mbwa mwishoni mwa mwaka jana nyumbani kwake.
Watu mbalimbali wamemtakia mapumziko mema na kuimboa familia ya Mzee Kingunge ipate nguvu katika kipindi hiki kigumu kwao wakiwepo, wasanii mbalimbali, pamoja na wanasiasa.